“Anaonekana Fiti Though” — My Story (Kufeel Sana, Kuongea Kiasi)

⏳ 2 Minutes Read • Men's Mental Health 

Photo: Tutanota

So, let me paint a picture: Mi ni yut wa 20s, Kenyan, morio — so basically hiyo inamaanisha life yangu lately imekuwa mainly kuambiwa, eti mara ooh:

 “Wewe sasa ni mwanaume.”

 “Usilie, deal nayo.”

"Feelings ni za mamas...” 

...and so on.

Na hiyo ndiyo imekuwa manual. Yaani, hakuwa na toolkit ya emotions. Society kazi ni kukuwa tu na expectations. Pressure ni real… na mara mob, ni trauma huwa inafuata baadae.

Nilianzisha hii page coz nilichoka kujifanya niko poa — na nilijua si mimi pekee niko hivo. Tuko wengi, of course, ni vile tu tumekuwa messed up tukiambiwa tu normalize silence. Na ni ufala bro.


Who I'm I Really❓(Apart from kuwa Overthinker Full Time)

Naitwa Keem. Mi ni bro wa kawaida tu, kama wewe. Nimekuwa stressed before, Yeah ! still at this age. Sometimes unaamkanga — unaangalia vile tu umesota, business ideas mingi mingi kwa akili.Dreams kibao, lakini means, ZERO🙁
Mara unaskia tu mwili haina mood, na saa hizo ndo kurauka.
Alafu, kashetani fulani kanakuambia uingie Instagram kidogo...Then Boom‼️
...Unaona kijana mdogo wa miaka fifteen akona Lamborghini, mwingine ashaenda vacation hizo sides za Maldives, mwingine ashaoa — alafu sasa kuna Mimi na wewe.
Kazi ni kudishi Fuliza na Okoa Jahazi...
Depression na anxiety inaingia...Wueh🤯
Na nime fake smile, but behind the scenes kichwa ni kuruka — silently.

...And so on.

Naandika juu inanisaidia ku-release. Naandika kuhusu men’s mental health — lakini si ile ya textbook ama ya therapist anakuambia “how do you feel today?”
Naandika venye inakujia kwa ground: raw, lost, messd up kidogo, na sometimes hadi na jokes. Ju tuseme ukweli — healing sio lazima ikuwe serious. Leo unajipata unaandika journal, kesho unabinge-watch cartoons za childhood juu dunia imekuwa noisy sana, saa zingine meditation 🧘‍♀️


Hii Space Ni ya Nani❓

Photo: Bykeem

Hii ni place ya wasee hujibu “Niko fiti” na ile smile ya kucover up pain.

Ni kwa maboyz (mostly 18 hadi 25)— lakini hata kama umepita hiyo bracket, na bado haujui kuongea kuhusu feelings zako… Karibu nyumbani bro 🙏

Hapa nayo utapata real talk:

◾ Heartbreaks bado hazijacheckiwa 💔
◾ Pressure ya kuwa successful kabla 25 💰
◾ Ile anxiety ya kukanyagia unaficha kila siku 😟
◾ Kuhakikisha therapy si ya wasee “wako na shida pekee” 👨‍⚕️
◾ Na mbona kuopen up haina maana umekuwa soft👊🏽

Mi hutoa stories zangu: zile poa 📈, na hata zile disappointing 📉...Zote Zote !



Mbona Hii Topic Inahold Weight 💪🏽

Kwa the modern society, “mwanaume” ni kuelewa kuprovide, kulinda… lakini si kufeel.

Tuna-normalize silence, alafu baadaye tunashindwa mbona tuko in pits. Suicidal thoughts. Na vitu kama hizo.

Lakini mi naamini tunaweza change.
One story at a time.
Tukishare vile tunafeel genuinely, tunaeza build place legit — yenye maboyz wanaruhusiwa kufeel, kukuwa broken, na kujiunda tena — bila aibu.

Na kama tutatupa ka dark joke ndani ya process, hakuna noma bro. Healing si lazima ikuwe boring 😁


So, Let Me Ask 🗨️

Ni kitu gani moja ya maana kuhusu kuwa mwanaume you feel hakuna msee aliwahi kuambia? Maybe since childhood?

Anguka nayo hapo kwa comments👇
Usi-overthink. Iseme vile tu iko.

You Never know… maybe kuna msee mahali hapo ako tu anangoja mtu aseme wa kwanza.

#MensMentalHealth101🗣️
#JiongeeBro

Post a Comment

1 Comments