When Having a Job Doesn’t Mean Freedom...The Mid-Broke Era

⏳ 3 Minutes Read • Unemployment

Photo: Freepik

Kuna ile phase fulani weird wasee wengi hupitia, kwa 20s zao (or maybe older)— ile time yaani ukiwa na job ama ukose, life kinda inakaa tu the same.

Umepata ka-job, of course — lakini salary inakuanga kama airtime ya week. Pesa yenyewe haiwezi survive hata zaidi ya siku tatu, na saa hizo ni Monthly salary...

Meanwhile, relatives wengine kwenu wameshaanza story za "buroti" (plot) na anga dowry. Lakini kwako hata kusave ni kazi, lazma ifuatwe na overthinking.

Na hii ndo inaitangwa the MID-BROKE ERA — ukona kazi yes, lakini bado uko broke vibaya sana...
hadi M-Pesa yako inakuangalia ni kama inakuuliza:

Bro, uko sure uko sawa?”

Kukosa Job nayo Huwanga Ngori
...In the First Place

Let’s keep it 100 — kukosa job as boychild ni mental torture ile mbaya. Hiyo experience Inakuwanga soul-draining mahn.

Kazi ni kuamka tu bila plan.
Everytime unafungua emails na hope fulani — ukingoja “We’re pleased to inform you…”
Lakini unapata tu spam na newsletters zenye hujui hata uli-sign up aje.

Unaingia websites za job daily.
Every post inataka “5 years of experience” na ni entry-level. Like, WTF ??

And the worst part?

Society huacha kukuchukulia serious.

Wewe ni grown, lakini hata relatives wako  wadogo wanakulenga bana.
Family gatherings nazo zinakaa job interview:

💬 “Nowadays unafanya kazi gani?”

Na wewe unasmile tu fakely:

💬 “Mi niko tu... na hustle flani hapa na pale.”
(Hapa = bed. Pale = múng'etho)


Then Job Inaingia... But Still, Society Inakuambia "You're Not Enough" 🤯

At last, unaget job. Labda ni freelance, labda ni retail... ama labda ni 8–5 (Ile yenye una-earn enough to survive but not enough to live... You get the point)

And then unajiambia:

At least sasa naweza hepa stress kidogo

But before your first payslip even lands, pressure inaanza:

“Anza kureserve ka plot.”
“Siz yako school fees ni next week.”
“Utaoa lini?”
“Invest sasa.”
“Save.”
BLAH BLAH BLAH ‼️

So, Ukiwa jobless wewe ni "Failure" and then ukishapata job, then you're not "Enough"... Kwani watu wanatakanga Nini surely 🤨 

You quickly realise: having a job doesn’t END the pressure — it UPGRADES it.


System Iko Cooked, Proper — Hatuwezi Kataa

Tuongee ukweli: system yetu ni scam.

Corruption imekula kila kitu hadi huduma hazifanyi kazi. Opportunities skuizi ni rare, na zikipatikana lazma ukuwe na connections... Taon !
Loans? Ni kama ni za watoto wa wakubwa pekee.
Capital? Iko wapi?
Financial literacy? Curriculum haijui hiyo word.
Gava support? Ama niache mchezo.

Wooi ! Akiamungu Ruto ni Saitan !

Yet bado society inakutegemea ku-figure out life peke yako.

Kukuwa kijanaa sai ni kama kupewa GPS imecrack, halafu unaambiwa:

Jitafutie success. Na usipotee.”

Hujui direction ni gani. Unajaribu kila kitu.
Leo ni online gigs, kesho ni betting, kesho kutwa ni YouTube, then mitumba biz.
...and so on.

Alafu sasa depression inaanza.

And in all that, society bado ina-shout:

“Wewe ni mwanaume! Be a provider!”

Provider kutoka wapi bro? Uko serious?


Guilt Nayo Inaingia Deep...

Photo: Freepik

Huwezi support mzazi, ama family in particular...
Huwezi spoil manzi yako...
Huwezi support bro yako mdogo...
Huwezi hata jinunulia chips mwitu bro...

Na hapo ndo unaanza kujihisi failure.
Even when trying your best, hii dunia itakufanya uonekane haufanyi enough.

Ukiscroll social media, inaonekana kila mtu ako na wins — trips, iPhones, relationships, investments...
Wewe  bado uko kwa struggle ya “Fuliza ama Hustler Fund?” 😔


So, Boychild Afanye Nini?
...Skiza Vizuri 📣

☑️Zima Kelele za Wasee — Sio Kila opinion iko worth attention yako bro.
Watu wengi hukupea pressure tu coz hawaelewi struggles zako, or maybe hawajazipitia .
Set boundaries. Usikubali 3rd party opinions zi-define life Yako.
Growth yako sio race.

☑️Appreciate Wins Kidogo kidogo:

Umepata ka-gig, hata kama ni 300 bob daily? Hiyo ni Win.
Umesend CVs tatu already? Win.
Umesoma financial tips online? Big Win.

Usingoje kuomoka ati ndo usherehekee progress.
Anza tu polepole...

☑️Learn as You Grow — Hii dunia hakuna msee alizaliwa na manual ya hustle. Kila mtu hauanza mahali.
Chukua free online courses. Skiza podcasts. Sema “Sijui” na uliza. Take advantage ya AI bro.
Hiyo yote ni learning — na ni ya maana.

☑️Worth Yako sio Wallet Yako — Wewe si job yako. Ama account balance yako. Ama pia ability yako kuprovide sai.

Wewe ni msee uko in progress — and that’s more than “Enough”...


Society Tuchoree.. 
Hii culture ya “kama mwanaume huprovide, wewe ni worthless” — inamaliza maboyz.

Wacha maboyz wawe human.
Wa-grow. Wa-fail na wa-try tena bila aibu.

...22-year-old hawezi nunua shamba na bado ana-struggle na Wi-Fi ya daily 10bob.

Relax society. Relax!


To every young man anakam across hii post:

✓ Huja-fail. Huja-chelewa. Huja-lost.

You’re building na zero tools, broken system, na very little support.
Lakini bado uko strong — unashow up, unajaribu, na bado una-dream.

That’s POWER.

Time yako inakam.
Hiyo hustle unapiga itajipa.
Your story bado inaandikwa — na itakuwa worth kusoma.


Ebu Tuongee Kiasi 💭
Umewahi skia umefanya your very best, lakini bado haifiki?
Drop story yako ama hata ka “same bro” hapo chini — tuko kimoja 💪

Post a Comment

1 Comments